• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Huenda Victor Wanyama akakatwa kiwango kikubwa cha mshahara wake

    (GMT+08:00) 2020-04-20 15:46:04

    Huenda kiwango kikubwa cha mshahara wa Victor Wanyama kikakatwa kufuatia ripoti kuwa chama cha wachezaji wa Major League Soccer (MLS) kinajadiliana na wachezaji kuhusu suala hilo kutokana na janga la virusi vya corona. Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars aliondoka Tottenham Hotspurs na kuyoyomea katika klabu ya Canada ya Montreal Impact Machi mwaka huu katika ofa ambayo inamshuhudia akitia kibindoni kima cha KSh15 milioni kila mwezi. Kwa mujibu wa ripoti ya ESPN, huku mapendekezo hayo yakikosa kuafikiwa rasmi, ligi hiyo inawaomba wachezaji kukubali kupokea 50% ya mishahara yao endapo mechi zitafutwa. Huenda asilimia hiyo ikabadilika kutoka na idadi ya mechi zitakazochezwa na pia michezo zitakazoandaliwa bila mashabiki kuhudhuria. Hata hivyo, wachezaji wanaopokea mshahara wa chini ya KSh10 milioni msimu huu hawatakatwa mishahara yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako