• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Viashiria mbalimbali vya uchumi wa China vyaboreka mwezi Machi

  (GMT+08:00) 2020-04-20 17:08:30

  Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China imesema, toka mwezi Machi, viashiria mbalimbali vya uchumi wa China vimeboreka, shughuli za kiuchumi zinarudi kwenye hali ya kawaida na kampuni za Marekani na Japan zilizopo China zimeongeza sana uwekezaji wao ikilinganishwa na mwezi Februari.

  Akizungumza na waandishi wa habati hii leo mjini Beijing, , mkuu wa idara ya uchumi wa kitaifa katika Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Yan Pengcheng amesema hivi sasa utaratibu wa uchumi unarudi kwenye hali ya kawaida, na katika msingi wa kudhibiti ipasavyo maambukizi ya virusi vya Corona, ikiwa ni kazi ya muda mrefu, sehemu mbalimbali zinarudisha shughuli za uzalishaji, biashara na masoko. Toka mwezi Machi, viashiria kama matumizi ya nishati ya umeme na kiasi cha bidhaa zinazosafirishwa zimeongezeka kidhahiri, na hali ya kupungua kwa ongezeko la uzalishaji kiviwanda na huduma pia inaboreka.

  Pia ujenzi wa miundombinu ya aina mpya umefuatiliwa hivi karibuni. Akizungumzia hilo, Wu Hao, mkuu wa idara ya uvumbuzi na maendeleo ya teknolojia ya juu katika Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China amesema, China itaimarisha kazi ya kuandaa mpango kwenye ngazi ya juu, kuboresha mazingira ya kisera, na kutekeleza vizuri ujenzi wa miundombinu, pia kuhimiza maendeleo ya miundombinu ya aina mpya.

  "Kuharakisha kukundamtandao wa 5G, kuboresha mtandao wa internet wa fiber broadband, na kuharakisha ujenzi wa kituo cha pamoja cha taifa cha data kubwa. Kufanya miundombinu ya jadi kuwa ya kidijitali na akili bandia hatua kwa hatua. Pia kupanga mapema miundombinu ya uvumbuzi."

  Kadri hali ya maambukizi ya virusi vya Corona inavyodhibitiwa nchini China, kampuni za nchi za nje zilizopo nchini humo zimeongeza kasi ya kurudisha shughuli za uzalishaji. Msemaji wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Yuan Da amedokeza kuwa, tangu mwezi Machi, kampuni za Marekani na Japan zimeongeza nia ya kuwekeza ikilinganishwa na mwezi Februari, na kwamba idara husika zitafanya juhudi kufanikisha miradi mikubwa inayowekezwa na kampuni za nje.

  "China itahimiza kwa uratibu na kuunga mkono miradi mikubwa inayowekezwa na nchi za nje. Miradi ya uzalishaji viwandani na huduma inayokidhi vigezo itashughulikiwa kwa utaratibu maalum wa kikazi, ambao unalenga kuinua kiwango cha huduma kwa miradi ya uwekezaji wa kigeni."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako