• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uingereza na Umoja wa Ulaya zaanza duru ya pili ya mazungumzo ya biashara

  (GMT+08:00) 2020-04-21 11:36:32

  Uingereza na Umoja wa Ulaya zimeanza duru ya pili ya mazungumzo ya biashara.

  Kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, pande hizo mbili zinafanya mazungumzo kwa njia ya video. Mazungumzo hayo yanayofanyika kuanzia tarehe 20 hadi 24, yatajadili masuala ya bidhaa, biashara ya utoaji wa huduma, mambo ya uvuvi, na kanuni za ushindani wa haki. Ajenda muhimu ya mazungumzo hayo ni mazingira ya ushindani wa haki, ushirikiano wa kisheria unaohusiana na mambo ya uchumi, muundo wa makubaliano na suala la mambo ya uvuvi, ambazo zinachukuliwa na mwakilishi wa mazungumzo wa Umoja wa Ulaya Bw. Michel Barnier kama ni sekta zenye maoni tofauti zaidi katika duru ya kwanza ya mazungumzo hayo.

  Vyombo vya habari vinakadiria kuwa, pande hizo mbili kutoa taarifa ya pamoja tarehe 16 na kutumai kufikia makubaliano ya mwanzo, kunamaanisha kuwa pande hizo mbili zitafanya mazungumzo mara kwa mara kuanzia tarehe 20, lakini kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona na athari zake kwa uchumi, mazungumzo hayo bado yanakabiliwa na changamoto nyingi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako