• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yachukua hatua za kupunguza ukosefu wa ajira unaotokana na virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-04-21 19:32:37

  Msemaji wa Wizara ya Rasilimali Watu na Huduma za Kijamii ya China Lu Aihong leo hapa Beijing amesema katika robo ya kwanza ya mwaka huu, China imetoa hatua mfululizo za sera za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, pia imetoa huduma za kijamii na kupunguza ukosefu wa ajira unaotokana na virusi hivyo. Aidha, imepanga kai za kutoa elimu ya ufundi stadi kwenye mtandao wa internet, jambo ambalo limeonesha ufanisi wake wa mwanzo.

  Takwimu zilizotolewa na Wizara hiyo zinaonesha kuwa, China ilishuhudia ongezeko la wafanyakazi milioni 2.29 mijini katika mwezi wa Januari hadi Machi, idadi ambayo ilipungua kwa watu laki 9.5 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo. Kiwango cha ukosefu wa ajira mijini kilipungua kidogo katika mwezi Machi na kuwa asilimia 5.9. Lu amesema, tangu mwanzo wa mwaka huu, China imetoa hatua mfululizo za sera na kutuliza ajira.

  "Serikali imehamasisha kampuni elfu 10 kutoa nafasi za ajira kwa watu laki tano, na kuhakikisha uzalishaji wa uhakika wa vifaa vya matibabu na bidhaa za mahitaji ya kila siku. Kusaidia kuwapeleka wafanyakazi vibarua kufanya kazi kutoka nyumbani na idadi ya waliosaidiwa ilifikia karibu milioni 5.9. Kurudisha bima ya ukosefu ajira yenye thamani ya Yuan bilioni 38.8 kwa kampuni milioni 3.02, na wafanyakazi waliofaidika walifikia milioni 80.76, idadi ambayo ni kubwa kuliko mwaka jana."

  Mkuu wa idara ya ujenzi wa ufundi stadi katika Wizara hiyo Zhang Lixin naye amesema, tangu mlipuko wa virusi vya Corona utokee nchini China, Wizara hiyo ilitekeleza mpango wa kutoa elimu ya ufundi stadi kupitia mtandao wa internet, na kuzindua kampeni ya kutoa elimu hiyo kwa bure kwa siku 100, jambo ambalo limepata mafanikio hadi sasa.

  "Hadi tarehe 17, Aprili, mikoa 31 imetangaza majina na tovuti za majukwaa 893 ya kutoa elimu ya ufundi stadi, na masomo yaliyotolewa yamefikia elfu 20, na yanajikita kwenye ufundi zaidi ya mia moja. Hivi sasa, watu milioni 5.9 wamejiandikisha kwenye majukwaa hayo kote nchini China. Hii imetoa mchango muhimu kwa shughuli za kurudisha uzalishaji na kutuliza soko la ajira."

  Kuhusu suala la kuhakikisha utoaji wa pensheni, mkuu wa idara ya bima ya pensheni katika Wizara ya Rasilimali Watu na Huduma za Kijamii Nie Mingjun amesema, hakuna shida katika kutoa pensheni, na kwamba bado kuna Yuan trilioni 5 za akiba ya pesa kwa ajili ya bima ya pensheni ya kampuni kote nchini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako