• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Manara amsifu Fei Toto wa Yanga

    (GMT+08:00) 2020-04-23 15:51:26

    Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa kiungo wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' ni mchezaji bora Mtanzania katika nafasi ya kiungo licha ya kuwa bado hajaonesha uwezo wake kwa asilimia 100. Akizungumzia uwezo wa kiungo huyo, Manara alisema kuwa Fei Toto anatakiwa kujitambua nini anahitaji katika maisha yake ya soka, kwa kuwa amejaaliwa kipaji kikubwa kuliko wachezaji wengi wazawa, lakini amekuwa akikwamishwa na vitu vidogo vidogo ambayo anatakiwa kuvifanyia kazi mapema ili kufikia kwenye kilele cha ubora wa asilimia 100. Amesema Fei Toto ni moja ya kiungo aliyejaaliwa uwezo mkubwa uwanjani, ndiyo maana hata kocha wa zamani wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike alimtabiria kuwa atakuja kufanya makubwa zaidi kwenye soka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako