• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaharakisha ujenzi wa nchi yenye nguvu kubwa ya hakimiliki za ubunifu

  (GMT+08:00) 2020-04-23 17:08:37

  Mkuu wa Idara ya Hakimiliki za Ubunifu ya China Shen Changyu leo amesema, mwaka jana idadi ya biashara ya hataza nchini China ilizidi elfu 3, na thamani ya biashara hizo ilizidi dola bilioni 131 za Kimarekani. Wakati huohuo, ushirikiano wa kimataifa katika hakimiliki za ubunifu pia umeimarika.

  Takwimu zinaonesha kuwa, idadi ya hakimiliki zinazomilikiwa na China imeongezeka kwa kasi. Kati ya mwaka 2007 na 2019, idadi ya hataza nchini China (isipokuwa Hong Kong, Macao na Taiwan) iliongezeka kutoka elfu 84 hadi milioni 1.86. Shen anasema

  "Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka jana, miji iliyopewa kipaumbele katika kujenga mfumo wa huduma za hakimiliki za ubunifu nchini China iliongezeka na kuwa 26. Majukwaa 9 ya uendeshaji wa hakimiliki za ubunifu yamesajili hakimiliki laki 1.21, na yana watumiaji rasmi laki 2.84. China imepata ufanisi mpya katika ujenzi wa mfumo wa uendeshaji wa hakimiliki za ubunifu."

  Hadi sasa China imeanzisha uhusiano wa kushirikiana na nchi zaidi ya 80 katika sekta ya hakimiliki za ubunifu, na imekuwa mshirika muhimu wa kutunga usanifu wa kimataifa na uendeshaji wa mambo ya hakimiliki za ubunifu duniani. Shen amesema, katika ushirikiano wa kimataifa wa hakimiliki za ubunifu, China inatilia maanani sana nchi zilizojiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  "Tumepanga miradi minane ya ushirikiano halisi na pande mbalimbali husika, ambayo imehusisha ulinzi wa hakimiliki za ubunifu, uchunguzi wa biashara, ujenzi wa uwezo wa kimsingi, kuongeza mwamko wa watu kuhusu hakimiliki za ubunifu. Hadi sasa miradi hiyo yote imepiga hatua muhimu. Wakati huohuo, idadi ya kuomba hataza kati ya China na nchi zilizojiunga na pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' imeongezeka sana, na ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta ya hakimiliki za ubunifu umehimiza ujenzi wa pendekezo hilo."

  Shen amesema, hivi sasa China inaharakisha kutunga mwongozo wa kimkakati wa ujenzi wa nchi yenye nguvu kubwa ya hakimiliki za ubunifu, ambao ni muhimu sana kwa kutimiza lengo la kuijenga China iwe nchi ya kisasa ya kijamaa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako