• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kituo cha matibabu ya virusi vya Corona cha Mombasa chazinduliwa

  (GMT+08:00) 2020-04-24 09:20:35

  Katika mikakati ya kupambana na virusi vya Corona duniani, nchi tofauti zimeweka mikakati tofauti ya kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

  Nchini Kenya kaunti ya Mombasa Gavana Hassan Joho amezindua kituo cha Matibabu ya virusi vya Corona na imeanza na vitanda 300, lakini inawezo wa vitanda 500.

  Gavana Joho amewahakikishia wananchi wake kuwa matibabu watakayo pokea ni mazuri kwani kituo hicho kiko na vifaa vyote vinavyohitajika kutibu mtu yeyote anayeugua ugonjwa wa Corona.

  Katika harakati za kupambana na Virusi hatari vya Corona Gavana wa Mombasa Hssan Joho amechukua hatua kadhaa kuweza kulinda wananchi wake kutoka na virusi hivi. Hii ni kupitia ujenzi wa kituo cha matibabu ya virusi vya Corona.

  katika maongezi yake kituo tayari kina vitanda 300 na kina uwezo wa vitanda 500.

  "Tunaanza na vitanda 300 lakini iko na nafasi ya kuweka vitanda hadi 500, tunaangalia hali ilivyo kama itatubidi kuongeza tutafanya hivyo"

  Serikali ya Mombasa ni moja wapo kaunti ambayo imejitolea kupambana na virusi hivi baada ya mji mkuu wa Kenya.

  Gavana amewaomba wananchi wa Mombasa kuwasaidia kupambana na virusi kuto kuenea kwa kujitokeza endapo unahisi maumivu ambayo yanaambatana na virusi vya Corona.

  "Tunafanya yote tuwezayo kuhakikisha tuna vituo vya kutosha kukulinda wewe, na kila mtu anachangia kwa njia moja au nyingine pia tunakuomba wewe hapo, wakati utapata dalili za ugonjwa huu au ugunduwe kuwa watu umewasiliana nao wanadalili za virusi hivi, jambo sahihi kwako ni kuja mbele na sisi hapa tuko tayari kusaidia"

  Watu wengi wamekosa kujitokeza wanapohisi dalili zqa virusi hivi, wengi wakiona haya au kufikiria jamii itawachukulia vipi, na wengine kuogopa mazingira ya karatini, Gavana amewahakikishia wananchi wake kuwa katika kituo cha matibabu ya Corona kuna mazingira mazuri na pia wameandaa vya kula maalum kwa ajili ya wagonjwa.

  "Kumekuwa na matukio pale watu wanapiga namba zetu zilizowekwa kwa wagonjwa wa virusi vya Corona na tunapochukua namba zao na kuwapigia wanakataa kushirikiana ujumbe na wambia watu hao Mombasa tumejianda vilivyo atatumetayarisha aina tofauti ya menyu kwa wangonjwa wetu wa virusi vya corona ili usiwe peke yako sio aibu kuwa kupatikana na virusi vya Corona unaweza kutibiwa na kutunzwa vyema na baadaye kuenda nyumbani kwako na kuishi maisha yako ya kawaida"

  Mombasa ikiendelea kuandikisha ongezeko kubwa zaidi kwa siku moja ya maambukizi ya virusi vya Corona maandalizi kambambe ya mewekwa kuweza kuzuia kuenea virusi vya Corona Kunti hiyo.

  katika kesi kumi na saba mpya watu kumi na mbili ni kutoka Mombasa kufikia sasa maambukizi yalioandikishwa nchini 320.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako