• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa vifaa vya matibabu kwa Nigeria

    (GMT+08:00) 2020-04-24 10:09:48

    Hafla ya kukabidhi vifaa vya matibabu vilivyotolewa na serikali ya China kwa Nigeria imefanyika jana huko Abuja, na kuhudhuriwa na balozi wa China nchini Nigeria Bw. Zhou Pingjian na mratibu wa rais wa Nigeria anayeshughulikia mwitikio wa COVID-19 na katibu mkuu kiongozi wa serikali ya Nigeria.

    Balozi Zhou amesema China itaendelea kubadilishana uzoefu wa kupambana na COVID-19 na Nigeria, na kutoa msaada kadiri iwezevyo kwa Nigeria kutokana na mahitaji yake. Pia amesema China ina imani kuwa Nigeria inaweza kushinda janga hilo.

    Mratibu wa rais wa Nigeria amesema vifaa vilivyotolewa na China vimesambazwa kwa hospitali mbalimbali, vituo vya karantini vilivojengwa kwa msaada wa China pia vimekamilika, na madaktari wa China pia wametoa msaada wa kiufundi kwa Nigeria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako