• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China awataka wananchi washirikiane kukabiliana kwa pamoja na janga la virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-04-25 19:21:59

  Rais Xi Jinping wa China ametoa wito kwa wananchi kujikuza kwenye taabu katika wakati huu wa janga la virusi vya Corona.

  Rais Xi ameyasema hayo alipokutana na walimu na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jiaotong cha Xi'an katika ziara yake mkoani Shaanxi.

  Chuo Kikuu hicho kinajulikana kwa historia yake ya kuhamia kwenye mji huu uliopo magharibi ya kati mwa China uliokuwa na mazingira magumu kutoka mji wa kisasa wa mashariki wa Shanghai katika miaka ya 50 ya karne iliyopita ili kuunga mkono maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya sehemu za magharibi mwa China, kitendo ambacho kimeelezwa kuwa ni "moyo wa kuhamia upande wa magharibi". Kiini cha moyo huu ni uzalendo na uwajibikaji, vitu ambavyo vimechangia sana maendeleo ya kasi ya China katika miongo kadhaa iliyopita.

  Kwa mujibu wa mpango, mwaka huu China inatarajiwa kukamilisha kazi ya kuondoa umaskini uliokithiri na kutimiza lengo la kufanikiwa kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote. Lakini maambukizi ya virusi vya Corona yaliyokuja ghafla yameleta changamoto kubwa kwa uchumi na jamii nchini China.

  Hata hivyo katika vita dhidi ya virusi vya Corona, wahudumu wa afya wa China, wahitimu wa vyuo vikuu, na raia wa kawaida wameonesha moyo huo wa uzalendo na uwajibikaji na kuisaidia China kushinda taabu, kupata ushindi na kutimiza malengo. Kama alivyosema mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Ghebreyesus, madaktari na wauguzi wa China waliopo mstari wa mbele wa kupambana na virusi vya Corona ni mashujaa wa kweli, na wamejitolea kwa kuungana na wenzao wa miji iliyoathiriwa vibaya na virusi hivyo ili kulinda dunia nzima.

  Katika vita dhidi ya umaskini uliokithiri, moyo huo pia umeoneshwa. Na ni kutokana na juhudi za pamoja za wachina wanaojitolea kwa ajili ya ujenzi wa taifa, watu zaidi ya milioni 800 wamefanikiwa kuondokana na umaskini katika miaka zaidi ya 70 iliyopita nchini China.

  Hivi sasa, virusi vya Corona bado vinaendelea kuenea kote duniani, na athari mbaya kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii zimezidi kuonekana. Katika wakati huu mgumu, moyo huu wa uzalendo na uwajibikaji sio tu unawapa moyo wachina katika kuendelea kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona bila kusita na kupata ushindi wa mwisho, bali pia utasaidia China kutimiza jukumu la maendeleo kama ilivyopangwa na kutimiza lengo la kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako