• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KASHFA: Moise Kean awashtua mabosi wake kwa kufanya sherehe ya siri wakati huu wa Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-27 09:19:36

    Klabu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza imesema kuwa imestushwa na taarifa kuhusu mshambuliaji wao Moise Kean kuvunja sheria ya kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima wakati huu wa kupambana na maambukizi ya Virusi vya Corona. Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo mwenye miaka 20 aliaandaa sherehe ya siri na kuwakusanya wageni kibao ambao asilimia kubwa inaelezwa kuwa walikuwa ni Wanawake. Nyota huyo ambaye anatajwa kuwa kwenye ubora wake msimu huu alifanya sherehe hiyo kwa siri jambo ambalo haliruhusiwi kwa kipindi hiki cha maambukizi ya Virusi vya Corona. Taarifa kutoka ndani ya Everton zinaeleza kuwa mabosi hao wameshtushwa na habari hizo hivyo uchunguzi ukikamilika adhabu za kinidhamu zitamhusu nyota huyo kwa kosa la kuvunja utaratibu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako