• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Wanyama ataka FKF ishauriane na FIFA kuhusu Amrouche

    (GMT+08:00) 2020-04-27 16:31:33

    Nahodha wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars na kiungo wa zamani wa Tottenham Hotspur, Victor Wanyama, amelisihi Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kufanya kila linaloweza kuhakikisha kwamba nchi hiyo inashiriki mechi zijazo za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar. Chini ya kocha Francis Kimanzi, Harambee Stars kwa sasa wanakabiliwa na hatari ya kutupwa nje ya michuano hiyo baada ya kushindwa kumfidia kocha Adel Amrouche Sh109 milioni kufikia Aprili 23, 2020 jinsi ilivyoagizwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA). FKF iliamrishwa kumlipa Amrouche kiasi hicho cha fedha baada ya kutimuliwa kwake Agosti 2014 kutokana na msururu wa matokeo duni. Pamoja na hayo, namna ambavyo mkufunzi huyo raia wa Algeria na Ubelgiji alivyotimuliwa ilikuwa kinyume na masharti ya mkataba kati yake na FKF.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako