• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • MASUMBWI: Bondia Floyd Mayweather asema amestaafu ndondi bali si kutengeza dola kadhaa

    (GMT+08:00) 2020-04-28 09:12:05

    Bondia Floyd Mayweather, amesema kuwa licha ya kutangaza kustaafu kupanda ulingoni kuzichapa, lakini anaweza kurejea tena ikimbidi kufanya hivyo. Bondia huyo alivuna mkwanja mrefu baada ya kumtwanga bondia Conor McGeorge 2017 ambapo inaelezwa kuwa alikunja pauni milioni 300 sawa na bilioni 855. Mpambanaji huyo ambaye ni kichaa wa saa, akiwa anamiliki saa zaidi ya 41 huku moja ikiwa ile iliyotengenezwa na Jacob & Co yenye thamani ya pauni milioni 14 ambayo ndiyo ghali zaidi. Amesema kama alivyosema mwanzoni kuwa amestaafu, lakini hajastaafu kutengeneza dola kadhaa, na kuhoji kuwa kama anaweza kuiburudisha dunia na kutengeneza dola milioni 600 kwa nini asirudi ulingoni?.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako