• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ndidi hana mpango wa kuchomoka Leicester

    (GMT+08:00) 2020-04-29 09:38:44

    Kiungo wa Leicester City, Wilfred Ndidi amekana taarifa kwamba anajiandaa kuachana na maisha ya King Power mwishoni mwa msimu huu. Ndidi amekuwa na kiwango bora kwenye kikosi cha Leicester City, ambapo msimu huu amefunga mabao mawili na kuassist mara moja katika mechi 29 alizocheza. Tetesi ni kuwa Manchester United inahitaji huduma yake, lakini Ndidi ambaye ni raia wa Nigeria amezima ndoto hiyo akisema hana mpango wa kwenda kokote kwenye dirisha linalokuja la usajili la majira ya kiangazi. Ndidi amecheza mechi 130 kwenye timu hiyo tangu alipojiunga nayo akitokea KRC Genk mwaka 2017, na mkataba wake wa sasa utamalizika Juni mwaka 2024.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako