• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SAKATA: Ronaldinho ahojiwa kwa mara ya kwanza toka aachiwe kwa dhamana, asema hakujua kama paspoti yake ni feki

    (GMT+08:00) 2020-04-29 09:41:25

    Nyota wa zamani wa FC Barcelona na AC Milan Ronaldinho amefanya mahojiano kwa mara ya kwanza toka akamatwe nchini Paraguay kwa tuhuma ya kukutwa na passport bandia. Ronaldinho, 40, katika mahojiano maalum na chombo cha habari cha ABC cha Paraguay amefunguka na kueleza kuwa hakujua kama Passport aliyokuwa nayo ni bandia na endapo siku akiachiwa uhuru kitu cha kwanza atambusu mama yake kwa furaha. Pia ameahisi kushirikiana na Mahakama kutoa ufafanuzi kuhusiana na hili na kuwa na imani mambo yatakuwa sawa na Mungu atasaidia kumalizika hivi punde. Ronaldinho amebainisha kuwa alipogundua kuwa anaenda gerezani ilimuumiza sana kwani hakuwahi kuwaza kwamba atakuja kuwa katika hali kama hiyo na katika maisha yangu yote amejaribu kwa kiwango cha juu kuwapa watu furaha kupitia soka yake. Hivi sasa Ronaldinho na kaka yake wapo nje kwa dhamana Paraguay wakiwa katika hoteli maalum ya nyota nne chini ya uangalizi mkali ili wasitoroke.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako