• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Afrika zashirikiana kwenye mapambano dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-04-29 17:58:41

    Nchi nyingi za Afrika zikiwemo Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Benin na Angola, zimeimarisha hatua zao za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona yanayoenea kwa kasi barani Afrika. China ikiwa ni mwenzi wa nchi za Afrika, imetoa misaada kwa bara hilo kupitia njia mbalimbali.

    Hivi karibuni, wataalamu wa matibabu wa China wametoa uzoefu wao kuhusu kinga na tiba ya COVID-19 kwa njia ya video kwa madakari na maofisa wa wizara za afya katika nchi mbalimbali za Afrika, ikiwa ni pamoja na Kenya, Misri, Morocco, Angola na Madagascar. Wataalamu na maofisa wa nchi hizo wameipongeza China kwa mafanikio iliyopata katika kudhibiti mlipuko wa virusi vya Corona na mchango iliotoa katika kulinda usalama wa afya ya umma duniani. Pia wamesisitiza kuwa uzoefu na hatua zilizochukuliwa na China ni mfano wa kuigwa kwa nchi za Afrika katika kudhibiti virusi hivyo.

    Mbali na kutoa uzoefu wake, serikali ya China na mashirika ya kiraia pia yametoa misaada ya vifaa vya tiba kwa nchi za Afrika. Maofisa wa nchi za Afrika waliohudhuria halfa za kupokea vifaa hivyo kutoka China, wamesema nchi zao zitatumia vizuri vifaa hivyo, kujifunza uzoefu wa China na kushirikiana na China, ili kuweza kushinda mapema mapambano hayo dhidi ya virusi vya Corona.

    China na Afrika zina historia ndefu ya ushirikiano kwenye sekta ya afya. Mwaka 1963, China ilipeleka timu ya kwanza ya madaktari nchini Algeria. Katika nusu karne iliyopita, China imetuma madaktari zaidi ya elfu 20 kwenda nchi zaidi ya 50 za Afrika, ikiwa ni sehemu ya msaada wa kimatibabu kwa nchi hizo. China pia ilitoa mchango muhimu katika kudhibiti milipuko ya magonjwa ya kuambukiza, ikiwemo Malaria, Kipindupindu na Ebola, iliyotokea barani Afrika. Mwaka 2014, China ilituma wataalamu na madakari elfu moja kwenda nchi za Afrika Magharibi, kuzisaidia kudhibiti mlipuko wa Ebola. Hivi sasa, timu za madaktari wa China walioko katika nchi mbalimbali za Afrika pia wanajizatiti kuzisaidia nchi hizo kuongeza uwezo wa kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.

    Ushirikiano huo kwenye nyanja ya afya ya umma, ni sehemu ya juhudi zinazofanywa na China na Afrika kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano kati yao kwa pande zote. China iko pamoja na Afrika, na itapambana bega kwa bege na ndugu wa Afrika, hadi virusi vya Corona vitakapotokomezwa barani humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako