• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • USAJILI: David Beckham amtaka Diego Costa ajiunge na timu yake ya Inter Miami

    (GMT+08:00) 2020-04-30 09:26:08

    David Beckham anataka straika wa zamani wa Chelsea, Diego Costa ajiunge na timu yake ya Inter Miami. Inter Miami, msimu huu imecheza mechi mbili kabla ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS) haijasimamishwa kutokana na janga la corona. Timu hiyo imepoteza mechi zote. Beckham ameanza juhudi za kuhakikisha straika huyo raia wa Hispania mwenye asili ya Brazil anajiunga na timu yake na tayari ameanza mazungumzo na wawakilishi wake. Costa ambaye ni straika wa Atletico Madrid hivi sasa, alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao walifika Marekani katika kipindi cha maandalizi ya kabla ya kuanza kwa msimu huu ambapo walicheza mechi kadhaa za kirafiki ikiwemo dhidi ya mastaa wa MLS. Beckham aliyewahi kutamba na klabu za Manchester United, Real Madrid na timu ya taifa ya England, ni miongoni mwa wamiliki wa klabu hiyo akiwa pamoja na Marcelo Claure na Masayoshi Son.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako