• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanasayansi wa China na Marekani waungana kutafuta chanzo cha virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-04-30 18:06:54

  Wanasayansi kutoka Marekani wanashirikiana na wenzao wa China katika kutafuta chanzo cha virusi vya Corona, licha ya baadhi ya wanasiasa wa Marekani kueneza uvumi kwamba virusi hivyo vilitengenezwa katika maabara mjini Wuhan.

  Mkurugenzi wa Kituo cha Kinga na kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza katika Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani Bw. Ian Lipkin anashirikiana na timu ya watafiti wa China inayoongozwa na Profesa Lu Jiahai wa Kitivo cha Afya ya Umma katika Chuo Kikuu cha Sun Yat-sen cha Guangzhou, kutafuta kama virusi hivyo vilitokea sehemu nyingine ya China kabla ya kugundulika kwa mara ya kwanza mjini Wuhan, mwezi Desemba mwaka jana.

  Lipkin amesema, utafiti huo unategemea zaidi msaada wa Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha China (CDC), ambayo amesema inapenda kujifunza zaidi kuhusu chanzo cha aina hiyo ya virusi, na kwamba wanabadilishana kila wanachojifunza na jamii yote ya wanasayansi.

  Profesa Lu amesema, wanashirikiana na mikoa na idara mbalimbali ili kutafuta chanzo cha virusi, na kuongeza kuwa utafiti huo ulianza mwezi Februari na matokeo yake yatatolewa baadaye mwaka huu. Amesema Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha China kimesaidia kuwaunganisha na hospitali nyingine na vituo vya CDC vya mikoa nchini humo, na kuiwezesha timu yake kufikia sampuli za damu kutoka benki ya taifa ya damu zilizotolewa kwa watu waliougua nimonia mwezi Desemba na hata kabla ya hapo.

  Profesa huyo amesema, hiyo ni sehemu muhimu ya kazi yao, ambayo kupitia hiyo wanatafiti kama virusi vya Corona vilikuwepo kwa binadamu kabla havijagundulika mjini Wuhan. Lu amesema, wanasayansi hao wa China na Marekani pia wanatafiti sampuli za damu za wanyamapori wa aina mbalimbali ambao wanahisi wanaweza kuwa chanzo cha virusi hivyo, na wanajaribu kuelewa ni kwa njia gani maambukizi yalitokea kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.

  Bw. Lipkin alikuwa sehemu ya timu ya kimataifa iliyochapisha waraka kuhusu chanzo vha virusi vya Corona katika jarida la Nature Medicine mwezi Machi, ambao ulijumuisha kuwa, virusi vya Corona viliingizwa isivyo halali na Kakakuona wa Malaysia na kilikuwa sana na kirusi cha SARS-CoV-2. Lakini waliweka kuwa hawana imani kuwa Popo ndio waasisi wa virusi vya Corona. Mapema mwaka huu, Lipkin alikwenda China na kuweka mikakati na wanasayansi na wataalam wa China kuhusu kuimarisha mahitaji ya msingi ya kisayansi kupunguza ugonjwa na vifo vinavyotokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako