• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: PSG na Gor Mahia zatawazwa mabingwa wa msimu wa 2019/20

    (GMT+08:00) 2020-05-01 09:36:15

    Shirikisho la soka Ufaransa (LFP) limetangaza rasmi kuwa klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa kuwa ndio Mabingwa wa Ligi Kuu nchini humo (Ligie 1) 2019/20. Maamuzi hayo yameafikiwa kwa kuzingatia msimamo wa sasa wa Ligi ulipofikia ndio unatambulika kama mwisho wa msimu. Hadi maamuzi hayo yanatoka PSG walikuwa wanaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Ufaransa wakiwa na pointi 68 wamecheza mechi 27 na zilikuwa zimesalia mechi 11, tofauti ya pointi 12 na Olympic Marseille waliopo nafasi ya pili kwa kuwa na point 56. Nalo Shirikisho la Soka la Kenya, (KKF) limesema kuwa hakuna matumaini ya kuendelea na ligi kwa hivi karibuni na matokeo yake, Gor Mahia wametajwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) Ligi Kuu ya Kenya ilisitishwa tangu mwezi Machi kutokana na janga la Covid-19 bila tarehe rasmi ya kurudi. Hadi wakati huo, Gor Mahia walikuwa wakiongoza msimamo wa ligi kwa pointi 54 baada ya kucheza mechi 23. Juzi Jumatano, Shirikisho la Soka la Afrika, (Caf), liliyaandika barua Mashirikisho ya soka kufafanua njia itakayo tumika kumaliza msimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako