• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyikazi wa mikahawa kupimwa corona kwa shilingi 2,000.

    (GMT+08:00) 2020-05-04 15:48:22

    Wamiliki wa mikahawa na hoteli wamepata afueni kidogo baada ya Waziri wa Afya Mutahi Kagwe kutangaza kuwa watatozwa ada kati ya Sh2,000 na Sh4,000 kwa kila mmoja wa wafanyikazi wao kupimwa virusi vya corona.

    Bw Kagwe aliiambia Kamati ya Bunge kuhusu Sheria Mbadala Alhamisi kwamba uamuzi wa kupunguza gharama hiyo ya upimaji katika hospitali za umma ulifikiwa baada ya wafanyabiashara hao kulalamika kuwa hospitali za kibinafsi zinatoza ada za juu za hadi Sh10,500 kupima mtu mmoja.

    Jumanne iliyopita, serikali iliiruhusu mikahawa kufunguliwa lakini kwa masharti makali yanayolenga kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona, kama vile wahudumu wa biashara hizo kupimwa kubaini hali yao ya afya.

    Wenye mikahawa na hoteli pia walitakiwa kuhakikisha kuwa wateja na wafanyakazi wanadumisha kanuni ya kutengana kwa umbali wa mita moja, kuwekwa kwa maeneo ya watu kunawa au kutumia vieuzi (sanitizers), wateja kupimwa joto, wamikili kuchukua vibali vipya kutoka kwa idara ya afya ya umma, miongoni mwa mahitaji mengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako