• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalam Afrika waendelea kupinga pendekezo la kufanyia majaribio ya chanjo ya corona barani humo

  (GMT+08:00) 2020-05-05 09:32:57

  Wataalam wengi wa kiafya barani Afrika wameendelea kupinga pendekezo la wanasayansi wa Ulaya kufanyia majaribio ya chanjo ya corona barani humo.

  Nchini Kenya Daktari Wanjala Wekesa, anasema kwanza nchi hizo zingefanya majaribio huko Ulaya ambako tayari kuna athari kubwa zaidi ya virusi hivyo ikilinganishwa na Afrika.

  Amesema mfano wa China wa kuthibiti virusi vya Corona umetokana na kufuatwa kwa sheria lakini sio chjanjo inayochukua muda mrefu kuzalisha.

  Daktari Wekesa anaona kuwa kwanza sasa dunia ingezingatia suluhu la haraka ambalo ni kuzuia kuenea kwa virusi hivyo kabla ya kuanza kutafuta suluhu la kudumu kama vile chanjo au tiba.

  Na wakati nchi za Afrika zikikabili virusi hivyo, kumeibuka pia wanasayansi wanaozalisha tiba kama vile nchini Madagascar.

  Wanasayansi nchini humo wametumia mmea aina ya Artemisia kuzalisha dawa hiyo.

  Hata hivyo, Daktari Wekesa amefafanua kuwa nchi zote zinafaa kufuata ushauri wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ambalo linasema kuwa hakuna ushahidi kuwa dawa hiyo ya Madagascar inaweza kutibu Covid-19.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako