• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yapaswa kuchunguzwa na jamii ya kimataifa kwa maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-05-05 18:17:33

    Baadhi ya wanasiasa wa Marekani hivi karibuni wameendelea kusambaza uvumi kwamba, virusi vya Corona vimetengenezwa na China katika maabara ya mjini Wuhan, na kudai kufanya uchunguzi wa kimataifa kuhusu jambo hilo. Lakini ukweli ni kwamba jamii ya kimataifa ikiwemo vyombo vikuu vya habari vya Marekani inaona kuwa, badala ya China, Marekani inapaswa kuchunguzwa kwa maambukizi ya virusi hivyo.

    Mhariri mkuu wa Jarida la The Lancet ambalo ni maarufu zaidi la udaktari duniani Richard Horton hivi karibuni amesema, Marekani haikujiandaa vizuri katika miezi ya Februari na Machi, hali ambayo imefanya idadi ya vifo kutokana na COVID-19 ndani ya wiki 8 izidi idadi ya vifo katika vita ya Vietnam iliyodumu kwa miaka 8. Gazeti la New York Times la Marekani pia limeshangaa na kusema, ikiwa nchi yenye nguvu zaidi ya matibabu duniani, Marekani imekuwa na idadi kubwa zaidi za watu walioambukizwa na virusi vya Corona na wale waliofariki kutokana na virusi hivyo. Licha ya hayo, Marekani imekuwa nchi inayoleta zaidi mambukizi hayo kwa nchi nyingine duniani.

    Swali ni kwamba, je, kwa nini Marekani imeshindwa vibaya na virusi vya Corona, na inapaswa kubeba majukumu gani kwa kuenea kwa virusi hivyo duniani? Kwa nini wanasiasa wa Marekani wanakwepa kuwajibika, wanaficha nini? Mambo hayo yote yanapaswa kuchunguzwa na jamii ya kimataifa.

    Kwanza, Marekani inatakiwa kuyaruhusu mashirika ya kimataifa ikiwemo Shirika la Afya Duniani WHO kuchunguza Maabara yake ya Utafiti wa Viumbe ya Fort Detrick. Hivi sasa kuna watu wengi wanaotaka Marekani kueleza sababu ya kweli ya kufunga maabara hiyo, na kufafanua kwamba kama maabara hiyo imetengeneza virusi vya Corona, na kusababisha maambukizi ya COVID-19 duniani au la.

    Pili, Marekani inapaswa kushirikiana na jamii ya kimataifa kuchunguza ugonjwa wa mafua usio wa kawaida uliotokea mwaka jana. Kutokana na takwimu zilizotolewa na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani ACDC, hadi mwishoni mwa Februari, mafua hayo yaliyoanzia Septemba mwaka jana yameambukiza watu zaidi ya milioni 30 nchini humo. Mkurugenzi wa ACDC Robert Redfield amekiri kuwa, sababu halisi ya vifo vya baadhi ya "wagonjwa wa mafua" ni COVID-19. Hivyo swali ni kwamba, kuna wagonjwa wangapi wa mafua ambao ukweli ni wagonjwa wa COVID-19? Na kesi ya kwanza ya maambukizi ya COVID-19 duniani ilitokea Marekani?

    Tatu, Marekani pia inatakiwa kushirikiana na jamii ya kimataifa kuchunguza wakati halisi wa kutokea kwa maambukizi ya mapema ya virusi vya Corona nchini humo. Mkuu wa Kaunti ya Santa Clara nchini Marekani Jeffrey Smith kwa kunukuu habari zilizotolewa na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha kaunti hiyo amesema, maambukizi ya virusi vya Corona huenda yalianza kutokea mwezi Disemba mwaka jana katika wilaya hiyo.

    China ina msimamo wa wazi kuhusu uchunguzi wa kimataifa dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona. Inapinga kuchukulia uchunguzi huo kama njia ya kuipaka matope China, na kuona kuwa, unapaswa kufanywa katika nchi zote zenye maambukizi yasiyo ya kawaida, kwa usawa na chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa, ili kujua chanzo halisi cha virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako