• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazindua roketi ya masafa marefu aina ya 5B

    (GMT+08:00) 2020-05-05 19:32:05

    China leo imerusha kwa mafanikio roketi ya masafa marefu aina ya Long March 5B iliyobeba kizazi kipya cha chombo cha anga kinachoongozwa na binadamu na mzigo kwa ajili ya majaribio katika anga ya juu.

    Kwa mujibu wa Mamlaka ya Safari za Anga ya Juu ya China CMSA, roketi hiyo imerushwa saa 12 jioni leo kwa saa cha China katika Kituo cha Kurushia Vyombo vya Anga ya Juu cha Wenchang.

    Mamlaka hiyo imesema, mafanikio hayo yamemaliza hatua ya tatu ya mpango wa China wa kujenga kituo cha anga ya juu.

    Baraza la Serikali la China na Kamati Kuu ya Kijeshi ya China zimetoa salamu za pongezi kwa mafanikio ya uzinduzi wa roketi hiyo.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako