• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi Duniani wameahidi kuchangisha Euro Bilioni 7.4 kwa ajili ya utafiti na kutengeneza chanjo dhidi ya virusi vya corona.

    (GMT+08:00) 2020-05-05 19:38:28

    Viongozi wa dunia wameahidi kuchangisha Euro Bilioni 7.4 kwa ajili ya kufanya utafiti na kutengeneza chanjo dhidi ya virusi vya corona.

    Serikali, wafadhili na mashirika ya kimataifa yameahidi kuchangisha fedha hizo.

    Viongozi wa dunia wamesema chanjo yoyote itakayopatikana itapaswa itolewe kwa wote na kwa bei ambayo wote wataweza kuimudu.

    Umoja wa Ulaya umeahidi kuchangia Euro bilioni moja. Ujerumani imesema itatoa Euro milioni 525 na Ufaransa itatenga Euro milioni 500. Nchi nyingine zilizoahidi kuchangia ni pamoja na Norway ambayo si mwanachama wa Umoja wa Ulaya bali ni mwenyekiti mwenza wa juhudi hizo.

    Mataifa zaidi ya 30, Umoja wa Mataifa, mashirika ya misaada, wakfu wa Bill na Melinda Gates, na taasisi za utafiti ni sehemu ya juhudi za kukusanya michango kwa ajili ya kupatikana kwa chanjo dhidi ya virusi vya corona.

    Mpaka sasa watu milioni 3 na nusu wameambukizwa virusi vya corona na zaidi ya laki mbili na elfu arobaini wamekufa duniani kote kutokana na COVID -19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako