• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Mike "Iron" Tyson kurudi tena ulingoni

    (GMT+08:00) 2020-05-07 08:47:59

    Kama ulifuta uwezekano wa kumuona tena Mike "Iron" Tyson ulingoni, basi ulikosea kwa kuwa bondia huyo kwa sasa yupo katika mazoezi makali ya kurudi ulingoni, akitaka kucheza pambano la raundi tatu hadi nne. Chini ya mkufunzi wake, Rafael Cordeiro, Tyson ameonekana kuwa mwepesi katika mazoezi yake hadi kumshangaza Cordeiro na hata mabondia wengine akiwemo mkali wa ngumi mchanganyiko, Khabib Nurmahomedov ambaye alipagawa baada ya kuona video fupi iliyowekwa na Tyson katika akaunti yake ya mtandao wake wa Instagram uliotetemesha watu zaidi ya milioni moja wakishangazwa na kasi yake. Tyson anatarajiwa kurudi ulingoni katika pambano maalum la kuchangisha fedha na litakuwa la raundi zisizozidi tano, lakini mpinzani wake bado hajajulikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako