• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Hersi Said amkataa Said Ndemla

    (GMT+08:00) 2020-05-07 17:04:20

    Mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM ambao wamejipanga kufanya Usajili mkubwa ndani ya klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said amesema hawana mpango wa kumsajili mchezaji yoyote kutoka Simba SC. Hersi ametoa msisitizo huo, kufuatia mipango ya klabu ya Young Africans kuendelea kuhusishwa na taarifa za kuwanyemelea baadhi ya wachezaji wa mabingwa hao wa Tanzania bara, huku jina la kiungo Said Ndelma likiongoza kwenye orodha ya wachezaji wanaohusishwa kutua Jangwani. Ndemla amekuwa akihusishwa na tetesi za usajili ndani ya klabu ya Young Africans, uvumi ambao umekuwa ukijitokeza kila msimu wa dirisha la usajili, unapowadia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako