• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Haile Gebrselassie ashauri adhabu ya kifungo jela kwa wanamichezo duniani wanaotumia dawa za kusisimua misuli

    (GMT+08:00) 2020-05-08 08:45:40

    Gwiji wa zamani wa riadha wa Ethiopia, Haile Gebrselassie (47) ameshauri adhabu ya kifungo jela nchini mwake kwa wanamichezo wanaotumia dawa za kusisimua misuli ianze kutumika duniani ili kukomesha tabia hiyo sugu. Gebrselassie ambaye kwa sasa ni Rais wa Shirikisho la Riadha Ethiopia (EAF) amesema iko haja kwa kila nchi duniani kuweka sheria kali ili kuwafanya wanamichezo kuwa na hofu ya kushiriki vitendo hivyo haramu. Mwanariadha huyo nyota wa zamani wa Ethiopia ambaye ameweka rekodi 27 tofauti katika mbio, amesema kuwa hamu yake ni kuona wanariadha wanashindana kwa haki. Gebrselassie kabla ya kustaafu riadha alifanikiwa kuvuna medali mbili za dhahabu katika mashindano ya Olimpiki huku akitwaa mataji manne katika mashindano ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako