• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UVUMI: Adebayor akanusha taarifa iliyosambaa kuhusu CAF, Mohamed Salah na Sadio Mane

    (GMT+08:00) 2020-05-08 08:46:26

    Mshambuliaji wa Togo, Emmanuel Adebayor (36) amekanusha kuhusika na taarifa inayoliponda Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) pamoja na washambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah na Sadio Mane. Taarifa hiyo ambayo imekuwa ikisambaa kwa kasi barani Afrika, inaonyesha Adebayor akiishangaa Caf kwa kutoa tuzo za Uchezaji Bora Afrika kwa wachezaji hao wakati hawastahili. Taarifa hiyo inasema "Caf inasimama kama Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika. Kwa Salah na Mane kushinda tuzo hiyo ni jambo baya. Tuzo inatakiwa kwa mchezaji anayecheza ndani ya Afrika". Hata hivyo Adebayor ameibuka na kujitetea kwa kusema hajawahi kuzungumza kitu kama hicho na taarifa hiyo imetungwa ikilenga kumchafua na kumgombanisha na Caf pamoja na nyota hao wawili. Ikumbukwe kwamba Adebayor ni miongoni mwa nyota waliowahi kushinda tuzo hiyo mwaka 2008

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako