• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakazi wa mitaa ya Eastleigh mjini Nairobi na mji wa kale Mombasa wahamia kwa ndugu zao baada ya kutangazwa kwa zuio la siku 15

  (GMT+08:00) 2020-05-08 10:03:03

  Tangu agizo la kutoingia na kutoka katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi na mji wa kale Mombasa kwa siku 15 zijazo, wengi wa watu kutoka mitaa hiyo wametorokea kwa jamaa zao.

  Jambo ambalo serikali imetaja kama njia moja ya kuhatarisha maisha ya wengi, hata hivyo Serikali imetoa onyo kali kwa wale wanaendelea kukaribisha watu kutoka maeneo yaliofungwa.

  Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema serikali imechukua hatua hiyo kutokana na ongezeko la visa vya maambukizi ya virusi vya corona katika mitaa hiyo.

  Kesi za virusi vya corona zikiendelea kuongezeka na marufuku ya kuingia na kutoka kuwekwa katika mitaa ilionekana kukuwa na maambukizi mengi, Serikali imewaonya watu dhidi ya kutoka katika mitaa hiyo ambayo amari ya kuingia na kutoka imewekwa kwa siku 15 zijazo.

  Lengo kuu lilkiwa ni kupunguza ama kushitisha maambukizi ama maenezi ya virusi vya corona.

  "Hakuna kuingia wala kutoka mtaa wa Eastleigh jijini Nairobi na Mji wa Kale ulioko Mombasa kwa siku 15 zijazo na pia masoko yote na mikahawa iliyopo ndani ya mitaa hiyo kufungwa kwa siku 15 zijazo kuanzia masaa ya saa moja jioni"

  Katibu Mkuu wa Tawala za Afya Rashid Aman amesema tangu amri ya kutoingia na kutoka kutangazwa katika mtaa wa Eastleigh na Mombasa Old Town siku ya Jumatano, watu wengine walionekana kutorekea mitaa jirani na mitaa ambayo watu wa Nairobi wametorekea ni south c na south B.

  "Tunafahamu kuwa kutokana na maagizo watu wengine wameamua kutoka makwao na kwenda maeneo jirani wacha ni waonye hatua hii ni ya hatari na mbaya kwa sababu ikiwa umeambukizwa virusi hivi bila kujua basi inamaanisha umehamisha shida kwa eneo linguine na kile umefanya ni kukuza kuenea kwa ugonjwa huu katika eneo hilo ambalo umehamia"

  Eastleigh sasa imethibitisha kesi 77 kuwa eneo hilo lililo na maambukizo mengi nchini Kenya wakati Old Town, Mombasa, ina kesi 57.

  Shughuli za uchukuzi mitaa hiyo miwili pia zimepigwa marufuku kwa muda wa siku 15, lakini, Bw Kagwe amesema watu wanaruhusiwa kusafiri ndani kwa ndani katika mitaa hiyo, hasa kununua bidhaa kwenye maduka

  Haya tu ni maoni ya watu kutoka katika mitaa hiyo iliyofugwa kwa siku 15 zijazo.

  Serikali imewaonya watu dhidi ya kutekeleza amri ya marufuku iliyotolewa katika maeneo ambayo kukuwa na visa vingi vya maambukizi ya virusi vya korona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako