• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kabananga adai hajapokea tuzo yake

    (GMT+08:00) 2020-05-08 16:56:25

    Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka DR Congo, Junior Kabananga amesema mpaka sasa hajapokea tuzo ya kiatu cha dhahabu, baada ya kuibuka kinara wa ufungaji bora wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2017). Kabananga ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Qatar SC ya Qatar, alifunga mabao matatu katika fainali hizo zilizofanyika nchini Gabon, na timu ya taifa ya Cameroon ilitawazwa kuwa mabingwa. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, amesema mpaka sasa hajapokea tuzo hiyo, na amewahi kuwakumbusha viongozi wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kupitia Shirikisho la Soka la DRC (FECOFA). Katika fainali za AFCON 2017, Kabananga aliiongoza timu yake hadi kufika robo fainali wakipoteza mbele ya Ghana. Magoli yake matatu yote alifunga katika hatua ya makundi dhidi ya Togo, Ivory Coast na Morocco.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako