• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Klabu zataja fedha kumalizia Ligi Kuu

    (GMT+08:00) 2020-05-08 17:30:02

    Baadhi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambazo hazina udhamini binafsi zimeanza kutafuta njia za kupata fedha za kumalizia mechi zilizopangwa kuanza katikati ya mwezi ujao. Hata hivyo, timu hizo pamoja na nyingine zilizoshiriki Ligi hiyo zinapokea mgao kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu ambao ni Vodacom, Azam TV na KCB. Timu hizo ikiwemo SIngida United, Coastal Union, Biashara United, Ndanda FC na Mbao FC, hutegemea zaidi fedha za wadhamini hao na viingilio vy mashabiki kwa mechi za viwanja vya nyumbani. Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amesema, wanakabiliwa na changamoto ya kukusanya si chini ya milioni 50 ili kuwawezesha kumaliza ligi kwa kucheza mechi tisa zilizosalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako