• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Kosgei kuamua kama atashiriki mbio za marathon za London ama Chicago mwezi Oktoba

    (GMT+08:00) 2020-05-08 17:30:30

    Mshikizi wa rekodi ya dunia ya mbio za Marathon raia wa Kenya, Brigid Kosgei yuko kwenye sintofahamu kuhusu mbio gani ashiriki itakapofika Oktoba, miezi mitano toka sasa. Mbio za Marathon za London ziliahirishwa kutoka April hadi October kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, lakini pia, mbio za marathon za Chicago zimepangwa kufanyika October 11. Kosgei ameeleza kupendelea kushiriki kwenye mashindano hayo yote, lakini inabidi afanye uchaguzi mgumu na kushiriki kwenye shindano moja. Amesema maandalizi yake kwa ajili ya mbio za Marathon za London ambako alikuwa anakwenda kutetea rekodi yake yalikuwa mazuri sana kwa kuwa alikuwa na chini ya miezi miwili kukamiliza mpango wake kabla ya kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako