• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua iliyoandikiwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari ya mji wa Wuhan kwa mwakilishi wa WHO nchini China Bw. Gauden Galea

    (GMT+08:00) 2020-05-08 18:43:31

    Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani nchini China Bw. Gauden Galea:

    Shikamoo! Mimi ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya mji wa Wuhan nchini China, nasomea shule ya Xu Guang ya mji wa Wuhan.

    Sasa usiku umefika, taa zinawaka hapa na pale, na uhai wa mji wa Wuhan unarejeshwa hatua kwa hatua. Siku chache zilizopita mimi na mama yangu tulipanda baiskeli karibu na Ziwa Donghu, hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kutembelea eneo lenye mazingira ya asili tangu maambukizi ya virusi vya Corona yalipoikumba Wuhan. Nafahamu mambo hayo yanayoonekana ya kawaida yanapatikana kutokana na kazi ngumu. Dunia ni kubwa, lakini hakuna mtu anayeweza kujitenga, virusi ni adui kwa binadamu wote. Mimi na wenzangu tuna matumaini ya pamoja ya kutoa mchango kwa ajili ya dunia yetu.

    Bw Galea, mimi na wanafunzi wenzangu tuliwahi kufanya shughuli za kutofautisha takataka, na tulikusanya pesa kwa kuuza takataka zinazoweza kutumiwa tena kama vile chupa za soda kwa ajili ya kuandaa shughuli za darasa letu, lakini sasa tunataka kutoa pesa hizo kwa Shirika la Afya Duniani, pia tunaahidi kuchangisha pesa tutakazozikusanya kwa njia hiyo kila mwaka kwa Shirika lenu. Vilevile tunatumai kutoa wito kwa vijana wote duniani kushirikiana kuwasaidia watu wanaohitaji msaada kadiri tuwezavyo.

    Sisi tukiwa mustakabali wa dunia, ni jukumu letu kulinda mustakabali wa dunia.

    Nakutakia afya njema!

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako