• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Marekani ina shauku ya kufungua nchi huku idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona ikifikia zaidi ya milioni moja

    (GMT+08:00) 2020-05-08 18:47:27

    Wakati idadi ya jumla ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani ikiongezeka na kufikia milioni 1.5, huku idadi ya vifo ikiwa zaidi ya elfu 75 mpaka kufikia jana jioni, serikali ya Marekani inajitahidi kufungua nchi hiyo kiuchumi, licha ya wasiwasi uliotolewa na wataalam wa afya ya umma na viongozi wa majimbo.

    Ripoti iliyotolewa na The Associated Press (AP) jana imesema, serikali ya Marekani chini ya rais Donald Trump imepuuza mwongozo wa kina uliotungwa na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani CDC, ukiwa na ushauri wa hatua kwa hatua kuhusu jinsi gani na lini inapaswa kufungua maeneo ya wazi wakati wa mlipuko wa virusi vya Corona.

    Kutokana na ripoti hiyo, waraka huo wa kurasa 17 uliopewa kichwa cha "Mwongozo wa Mfumo wa Kutekeleza Ufunguaji wa Marekani" ulifanyiwa utafiti na kuandikwa ili kuwasaidia viongozi wa dini, wamiliki wa biashara, wakufunzi na maofisa wa serikali kuu na serikali za mitaa wanapojiandaa kufungua upya maeneo yao.

    Ofisa mmoja wa CDC ambaye hakutaka kuwekwa wazi alinukuliwa na ripoti hiyo ya AP akisema, waraka huo ulitarajiwa kuchapishwa hii leo, lakini wanasayansi wa CDC waliambiwa mwongozo huo kamwe hautachapishwa.

    Gazeti la New York Times limesema, mwongozo huo, ambao CDC iliuwasilisha Ikulu ya Marekani wiki mbili zilizopita ukiwa kama muswada, ulitarajiwa kusaidia majimbo, serikali za mitaa na wafanyabiashara kuchukua hatua zitakazosaidia kuzuia kuenea kwa virusi wakati wakifungua biashara zao, kama vile kutumia vyombo vinavyotupwa baada ya kutumika mara moja kwenye migahawa. Lakini taasisi kadhaa za serikali, ikiwemo Wizara ya Kazi na Ofisi ya Haki za Rais iliyo ndani ya Wizara ya Afya na Huduma za Jamii, zilipinga na kusema zitaathiri biashara na uchumi, na unagusa sana nyumba za ibada.

    Rais Trump alieleza nia yake ya kufungua tena uchumi wa nchi hiyo Alhamisi mchana katika video iliyorushwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, ambapo alisema wananchi wanataka nchi hiyo ifunguliwe, na serikali inataka kufanya hivyo lakini kwa njia salama. Pia amesema, uchumi wa Marekani utarudi tena kwa nguvu zaidi, na utafufuka haraka kuliko inavyotarajiwa.

    Zaidi ya majimbo 20, mengi yakiwa katikati ya nchi hiyo, yameanza kufungua biashara zao hatua kwa hatua, yakiruhusu baadhi ya biashara zisizo za muhimu sana kuendelea na kazi.

    Gavana wa Jimbo ya New York Andrew Cuomo amesema, hawezi kupoteza maisha ya watu kwa ajili ya kufufua uchumi, na kuongeza kuwa mazingira ya sasa haiwezekani kuwaambia Wamarekani wako tayari kupoteza maisha ya watu wangapi ili kufufua uchumi wa nchi yao. Ameongeza kuwa, hakuna mtu atakayetolewa kwenye nyumba yake kwa kushindwa kulipa kodi mpaka Agosti 20, kwa kuwa watu wengi wameathirika kiuchumi kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

    Wizara ya kazi nchini Marekani imesema, zaidi ya Wamarekani milioni 33 mpaka sasa wamewasilisha madai ya kutokuwa na kazi tangu mlipuko wa virusi vya Corona ulipotokea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako