• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndege ya Kenya Airways yawasili na wakenya waliokwama Mumbai na Guangzhou

    (GMT+08:00) 2020-05-08 20:21:10

    Ndege ya shirika la Kenya- Kenya Airways imewasili katika uwanja wa ndege ya Jomo kenyatta ikiwa na abiria wakenya ambao walikuwa wamekwama kutokana na janga la Corona katika miji ya London, Mumbai na Guangzhou. Ndege hiyo ilianza safari za kuwasafirisha wakenya kuanzia tarehe 4 mwezi huu kwa ndege aina ya Boeing 787 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 335. Ndege ya kutoka Uingereza iliwasili tarehe 4 huku za Mumbai na Guanzhous zikiwasili tarehe 7 na 8 mtawalia. Awali shirika hilo la ndege lilinukuliwa likisema kuwa abiria wa Uingewreza wangelipa dola 500 kwa tiketi moja huku wale ambao wamekwama katika miji ya Mumbai na Guangzhou walitakiwa kulipa dola 430 na 750 mtawalia. Hata hivyo wageni hao walitakiwa kulipia gharama ya vipimo vyao vya Covid 19 katika maabara ya Lancet hapa mjini Nairobi.Kwa kawaida gharama ya tiketi ya usafiri wa kwenda na kurudi kati ya Kenya na London huwa ni kati ya dola 964 na 482.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako