• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Dili la Aubameyang kwa Madrid litalazimika kusubiri kwanza

  (GMT+08:00) 2020-05-11 09:22:59

  Klabu ya Real Madrid imeripotiwa kutaka kusubiri hadi Juni 15, ili kufanya maamuzi ikiwa itamsajili straika wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ama la. Miamba hiyo kutoka La Liga ni miongoni mwa klabu zinazoikimbizia saini ya straika huyo wa Arsenal ambaye amebakiza miezi 13 kwenye mkataba wake wa sasa. Aubameyang anaripotiwa kuwa hana mpango wa kutaka kuongeza mkataba mpya Arsenal na badala yake anafikiria kuondoka pale mkataba wake utakapomalizika, ikiwa Arsenal hawatovunja benki ili kumpa dau nono litakalomshawishi. Ingawa Madrid inahitaji kumsainisha mchezaji huyo, lakini itawahitaji kusubiri hadi katikati ya mwezi ujao ili kujua, ikiwa watamsainisha nyota huyo ama hawatamsainisha. Taarifa kutoka Hispania zinadai kwamba Madrid inahitaji kufanikisha dili hilo kwa kufanya mabadilishano ya wachezaji ambapo, Dani Ceballos ni mmoja wa wachezaji wanaotajwa kwenye dili hilo. Hii inaelezwa kwamba ni kutokana na timu hiyo kuathiriwa kiuchumi na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona. Pia kuna taarifa zinazodai kuwa Madrid wanajua kwamba kukamilisha dili hilo kwa mabadilishano ya wachezaji haitakuwa rahisi hata kidogo, hivyo wanatazamia kuandaa ofa ya pauni milioni 40, ili kuishawishi zaidi Arsenal.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako