• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Djibouti yatoa nishani ya kitaifa kwa wataalamu wa matibabu wa China

    (GMT+08:00) 2020-05-11 09:57:34

    Waziri Mkuu wa Djibouti Bw. Abdoulkader Kamil Mohamed ametoa nishani ya kitaifa ya "Siku ya Uhuru ya tarehe 27 Juni" kwa wataalamu 12 wa kikundi cha matibabu kilichotumwa na serikali ya China, kutokana na mchango wao wa kuisaidia Djibouti kukabiliana na janga la COVID-19.

    Bw. Kamil ameishukuru serikali ya China kwa uungaji mkono wa dhati kwa Djibouti katika kupambana na janga hilo, na kuthamini sana mwongozo uliotolewa na kikundi cha watalaamu wa China katika kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, na kusema kuja kwao kumeimarisha zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Balozi wa China nchini Djibouti Zhuo Ruisheng, amesema kutolewa kwa nishani hiyo sio tu ni fahari ya kikundi hicho, bali pia ni ishara ya urafiki mkubwa kati ya watu wa China na Djibouti, na China inapenda kuendelea kushirikiana na Djibouti kupambana na janga la COVID-19, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako