• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Otiato Wafula ana matumai juu ya Mikutano miwili ya China

    (GMT+08:00) 2020-05-11 10:02:22
    Kongamano kubwa la vyombo vikuu vya kisheria nchini China maarufu kama "Mikutano Miwili" au "Two Sessions" litafanyika kuanzia tarehe 22 mwezi huu.

    Kongamano hili hulileta pamoja Bunge la China (Kongamano la Watu la Kitaifa-NPC) na Baraza la Mashauriano la Kisiasa nchini humo (CPPCC).

    Mikutano hii hufanyika kila mwaka,na huwa hasa na lengo la kuweka ajenda ya Rais ya mwaka unaofuata kwa China na kwa ulimwengu.

    Mtaalamu na Mhadhiri wa Soshiolojia na Siasa ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Kenyatta Dkt Otiato Wafula anasema kuwa katika mkutano wa mwaka huu ambao uliahirishwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona,na ambao utafanyika kwa njia ya video,mbali na serikali ya China kuzungumzia malengo yake ya mwaka unaofuata inafaa kuueleza ulimwengu na kujitakasa kuhusu tuhuma inazorushiwa na Marekani kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

    Aidha Dkt Otiato anasema mfumo wa kisiasa wa China umesaidia sana kwa nchi hiyo kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Corona kwa ufanisi na kwa muda mfupi,kutokana na watu kutii maagizo ya serikali na pia serikali kuwekeza nguvu nyingi katika kuhakikisha ugonjwa huo unadhibitiwa.

    Wakati huo huo Dkt Otiato amesema mataifa mengine yanafaa kujifunza kutoka mfumo wa kisiasa wa China wa kuwashirikisha wananchi na kuwafanya kuwa na utaifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako