• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Bei ya malimao, vitunguu swaumu yapanda

    (GMT+08:00) 2020-05-11 19:03:33
    Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema mabadiliko ya fasiri za bei ndani ya miezi miwili, yameongezeka kutokana na kupanda kwa bei ya baadhi ya bidhaa ikiwamo malimao na vitunguu swaumu, ambazo zinatumika kujifukiza kukabiliana na virusi vya corna.

    Haya yamebainishwa na kaimu mkurugenzi wa Sensa ya watu na takwimu za jamii wa ofisi hiyo, Ruth Minja. Kulingana nae, mfumuko wa bei kwa mwezi Aprili 2020, umepungua hadi asilimia 3.3, kutoka asilimia 3.4, kwa mwaka ulioishia mwezi Machi 2020.

    Aliongeza kwa kusema kwamba, kipindi kati ya Machi na Aprili, 2020, fahirisi za bei zimeongezeka asilimia 0.4 kutokana na uhitaji mkubwawa bidhaa hizo kuongezeka, ikilinganishwa na miezi 12 iliyopita.

    Kuhusu mfumuko wa bei, mkurugenzi huyo alisema kupungua huko kumetokana na kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa kipindi hicho kupungua, kwenye bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

    Kuhusu nchi za Afrika Mashariki, alisema kwa kenya mfumuko wa bei kwa kipindi hicho umeongezeka kidogo hadi asilimia 5.62 kutoka 5.51 kwa mwezi ulioishia Machi , 2020.

    Kwa upande wa Uganda, mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili 2020, umeongezeka hadi asilimia 3.2 kutoka 3.0 kwa mwaka ulioishia Machi 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako