• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TANZIA: Kiungo wa Atalanta ya Italia Andrea Rinaldi afariki dunia kwa tatizo la ubongo

    (GMT+08:00) 2020-05-12 08:34:12

    Kiungo wa Atalanta ya Italia Andrea Rinaldi, amefariki dunia kutotakana na matatizo ya ubongo aliyoyapata wakati akifanya mazoezi mepesi nyumbani kwake. Matatizo hayo yalianza Ijumaa wiki iliyopita. Rinaldi aliwahi kuwa sehemu ya kikosi chipukizi cha Atalanta kwa kipindi kirefu na amewahi kuchezea kikosi cha Legnano katika soka ya daraja la chini nchini Italia. Baadhi ya vyanzo kama shirika la Ansa vinasema amekuwa mali rasmi ya Legnano baada ya kununuliwa. Hata hivyo baadhi vimesema amekuwa huko kwa mkopo msimu huu. Kwa upande wao, viongozi wa kikosi cha Legnano walisema kifo cha Rinaldo kimekuwa pigo kubwa kwao. Legnano ambao walithibitisha pia chanzo cha kifo cha Rinaldi, walisema mchezaji huyo aliwaarifu kwamba alikuwa hajihisi vizuri kwa kipindi cha siku tatu ila hapakuwa na lolote kubwa ambalo wangeweza kumfanyia. Vyombo vya habari nchini Italia viliripoti kwamba Rinaldo aliaga dunia akitibiwa katika hospitali ya Varese asubuhi ya Mei 11, 2020. Rinaldi aliingia katika usajili rasmi na Atalanta akiwa na umri wa miaka 13 pekee na akaichochea klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A) kunyanyua ubingwa wa Super Cup kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17 mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako