• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • WHO yahimiza kulegeza hatua za kukabiliana na COVID-19 taratibu na hatua kwa hatua

  (GMT+08:00) 2020-05-12 09:28:35

  Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Ghebreyesus jana kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, hivi sasa nchi nyingi zinalegeza hatua za kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19, ili kufufua uchumi, na mchakato huu utakuwa na utatanishi na matatizo mengi. WHO inazitaka nchi hizo zifanye hivyo taratibu na hatua kwa hatua.

  Bw. Tedros amesema hadi sasa idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona duniani imezidi milioni nne. Hatua zilizochukuliwa na nchi mbalimbali zimepunguza kidhahiri kasi ya maambukizi ya virusi hivyo, na kuokoa maisha ya watu wengi. Lakini hatua hizo pia zimeleta athari mbaya kwa uchumi, hivyo zinapaswa kulegezwa hatua kwa hatua. Anasema,

  "Kwa hiyo, ili kulinda ajira wakati wa kuokoa maisha ya watu, ni muhimu kulegeza hatua za kukabiliana na COVID-19 taratibu na hatua kwa hatua. Hivyo tutafufua uchumi wakati tunachukua tahadhari dhidi ya virusi vya Corona. Na kama maambukizi yakiongezeka tena, tutachukua hatua haraka iwezakanavyo."

  Mkurugenzi mtendaji wa mipango ya dharura ya afya wa WHO Michael Ryan, ametahadharisha kuwa virusi vya Corona bado havijatokomezwa, hata kwenye nchi zenye maambukizi machache, kuna uwezekano wa kulipuka tena kwa COVID-19. Anasema,

  "Nchi nyingi zimeongeza uwekezaji mfululizo, ili kujenga uwezo wa afya ya umma. Lakini nchi nyingine bado hazijafanya hivyo. Tunapaswa kuhakikisha kuwa kila nchi inachukua hatua ipasavyo, na kufanya uchunguzi wa kiafya, ili kupata fursa ya kuepuka wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya Corona."

  Bw. Tedros amesema kufuatia kulegazwa kwa hatua za kukabiliana na virusi hivyo, maambukizi mapya yanaweza kuongezeka, na kuleta changamoto mpya. Amezipongeza China, Korea ya Kusini na Ujerumani kwa kuchukua hatua madhubuti za kudhibiti hali hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako