• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: La Liga sasa kuanza tena Juni 12

    (GMT+08:00) 2020-05-12 15:45:26

    Rais wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga), Javier Tebas amefichua mipango ya kuanza tena kwa Ligi hiyo msimu huu Juni 12. Kwa mujibu wa kinara huyo, kwa sasa wanajitahidi kuhakikisha kwamba pana uwezekano wa "asilimia sufuri" wa mchezaji au afisa yeyote wa soka ya La Liga kupata virusi vya corona pindi kivumbi hicho kitakapoanza tena kwa pamoja na kile cha Daraja ya Kwanza (Segunda). Vinara wa klabu zote 20 za La Liga walianza kuwapima wachezaji wao wiki jana huku mipangilio ya kurejelewa kwa mazoezi na mechi kusakatwa ndani ya viwanja vitupu bila mashabiki ikishika kasi. Tebas ameshikilia kwamba mechi za ligi nyinginezo za madaraja ya chini zitaanza kwa wakati mmoja (Juni 19) huku mechi za kitaifa zikiratibiwa kurejelewa Julai 31 ili kalenda ya soka ya Uhispania iwiane na ratiba ya Shirikisho la Soka Duniani na Shirikisho la Soka la Bara Ulaya ambalo limetaka fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) kupigwa kufikia mwisho wa Agosti 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako