• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Waagizaji wameanza kutumia usafiri wa maji na reli kwa ufikaji wa haraka na salama wa bidhaa zao

    (GMT+08:00) 2020-05-12 20:49:10
    Waagizaji wameanza kutumia usafiri wa maji na reli kwa ufikaji wa haraka na salama wa bidhaa zao kufuatia kuongezeka kwa kesi za virusi vya corona kwa madereva wa lori.

    Shirika la Reli la Uganda lilikabidhi jumla ya lita 1,020,000 za mafuta ya Petroli iliokuja kwa njia ya maji kutoka Kisumu Ijumaa.

    Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Reli la Uganda, Bwana Charles Kateeba amesema reli ya Uganda inapanga kuleta meli nyingine katika wiki tatu zijazo ambayo itaongeza uwezo wake wa kuagiza lita milioni 13 hadi 15 za mafuta kwa mwezi.

    Kulingana na takwimu za serikali iliyotolewa mnamo 2017, Waganda hutumia zaidi ya lita milioni tano za mafuta kila siku.

    Waziri wa Biashara, Bi Amelia Kyambade, amesema serikali itaanza kuagiza mafuta kwa kutumia reli na usafiri wa maji ili kupunguza idadi ya madereva wa malori ya kubeba mizigo wanaoingia nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako