• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ruhsa kufanya mazoezi ya pamoja Italia

    (GMT+08:00) 2020-05-13 15:57:30

    Klabu za soka nchini Italia zimepewa tuhusa ya kuanza kufanya mazoezi ya pamoja kuanzia mwanzoni mwa juma lijalo (Mei 18), kabla ya kuanza rasmi kwa ligi ya Serie A, na ligi nyingine nchini humo. Shirikisho la Soka nchini Italia FIGC limetoa taarifa hizo, kufuatia Serikali ya nchi hiyo kutangaza utaratibu wa klabu za michezo kurejea katika utaratibu wa kufanya mazoezi ya pamoja, kufuatia ahuweni ya maambukizi ya virusi vya Corona. Kabla ya agizo hilo, wachezaji wa soka na michezo mingine nchini Italia walikuwa wakifanya mazoezi binafsi nyumbani kwa kuhofia kasi ya maambukizi ya virusi vya Corona, ambayo ilikuwa juu nchini humo. Timu maalum ya utafiti ya kisayansi ambayo ipo chini ya Serikali, inaendelea kufanya utafiti wa kina, ili kujiridhisha hali halisi ya maambukizi ya virusi vya Corona, ambayo hata hivyo yameripotiwa kupungua kwa kiasi kikubwa. Majibu ya timu hiyo yanatarajiwa kutumika kama nyenzo ya kutoa ruhusa kwa viongozi wa shirikisho la soka nchini Italia (FIGC), kuendelea na ligi ama kusitishwa kwa msimu huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako