• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mtibwa Sugar yaweka wazi kuwa Humud hang'oki

    (GMT+08:00) 2020-05-13 15:58:00

    Licha ya kuhusishwa sana na mipango ya usajili ndani ya Young Africans, uongozi wa Mtibwa Sugar umesema hauna mpango wa kumuacha kiungo wao mkabaji Abdul-halim Humud. Msemaji wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema Humud bado ana mkataba na wakata miwa hao na hawafikirii kumruhusu akajiunge na Young Africans au timu nyingine yoyote hapa nchini. Amesema Humud ni mchezaji muhimu wa timu hiyo, na hawafikirii kumuacha akajiunge na timu yoyote hapa nchini labda apate nafasi nje ya nchi. Kifaru amesema Humud ni mfano wa kazi ambayo Mtibwa Sugar wamekuwa wakiifanya kwa miaka mingi kuimarisha viwango vya wachezaji pamoja na kuibua wachezaji wapya. Mtibwa Sugar ndio mabingwa wa ligi ya soka ya vijana wakiwa na timu imara za U17 na U20. Katika kikosi chao kinachoshiriki ligi kuu wanatumia wachezaji wengi wanaopita kwenye akademi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako