• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Sweden yaongeza sharia zaidi kwa wanariadha kutoka Kenya na Ethiopia

    (GMT+08:00) 2020-05-13 15:58:20

    Wakati wasiwasi ukiongezeka kuhusu kanuni za kudhibiti matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku, wanariadha kutoka Kenya sasa watakabiliwa na uchunguzi mkali kabla ya kushiriki kwenye mashindano nchini Sweden. Hatua hii imekuja baada ya Shirikisho la Riadha la Sweden kusema kwamba wanaimarisha sheria kwa wanariadha ambao wanafanya mazoezi katika nchi ambako vipimo vilivyochukuliwa kabla ya mashindano sio vya kisasa, huku Kenya na Ethiopia zikiwa katika kundi hili. Habari zinasema, katibu mkuu wa Shirikisho hilo Stefan Olsson ameeleza wasiwasi wake kuhusu uwezo wa vipimo vya kugundua matumizi ya dawa hizo zilizopigwa marufuku kwa wanariadha katika nchi za Kenya na Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako