• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Benki Kuu ya Tanzania (BoT), yaweka sera kukabiliana na athari za corona

    (GMT+08:00) 2020-05-13 20:36:00
    Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imetangaza hatua sita za kisera zilizochukuliwa kukabiliana na athari za corona kwenye benki ikiwa ni pamoja na kupunguza riba, amana, hati fungani na dhamana.

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka kw benki hiyo uamuzi huo umefikiwa na kamati ya sera ya fedha ya Bodi ya BoT na kutoa ahueni kwa taasisi za fedha.

    Ilibainisha kuwa lengo la hatua hizo ni kudumisha uthabiti wa sekta ya fedha na upatikanaji wa huduma za fedha nchini.

    Hatua zilizochukuliwa ni kushusha kiwango cha chini cha kisheria cha sehemu ya amana kinachotakiwa kuwekwa BoT kutoka asilimia saba hadi sita, kuanzia Juni 8, mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako