• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Harlequins yapania kufanya makubwa msimu ujao kwa kuongeza nguvu mpya

    (GMT+08:00) 2020-05-14 08:31:42

    Kikosi cha Kenya Harlequins kimemsajili aliyekuwa mwanaraga matata wa Homeboyz, Mark Wandetto kwa ajili ya kampeni za msimu ujao wa Ligi Kuu ya Kenya Cup. Winga huyo alikuwa miongoni mwa wanaraga tegemeo katika timu ya taifa ya wachezaji saba kila upande, Shujaa, chini ya kocha wa zamani wa kikosi hicho, Paul Murunga. Wandetto anajiunga na Quins siku chache baada ya kikosi hicho kumnasa pia Leroy Mbugua kutoka Blak Blad ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Anatazamiwa kuonesha makali yake kwa mara ya kwanza katika michuano ya taifa ya Sevens Circuit mnamo Julai au Agosti 2020. Wandetto amekuwa mhimili wa Homeboyz kwa kipindi cha misimu miwili iliyopita. Kwa mujibu wa Michael Wanjala ambaye ni mwenyekiti wa Quins, ujio wa Wandetto utakuwa kiini cha kufufuka kwa makali yao kadri kikosi chao kinavyojiandaa kujinyanyua katika msimu wa 2020-21 baada ya kuambulia nafasi ya tisa msimu huu. Quins wanajivunia idadi kubwa ya wanaraga makinda ambao wanalenga kuwapandisha kutoka akademia hadi kikosi cha kwanza. Katika kivumbi cha msimu huu, Quins walisajili ushindi katika mechi tano na kupoteza jumla ya michuano 11 katika matokeo yaliyowashuhudia wakijizolea alama 28 pekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako