• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magari ya mizigo yanayokwenda Mombasa kutoka Tanzania yakwama mpakani, Mkuu wa mkoa wa Tanga atoa wito wa ushirikiano

    (GMT+08:00) 2020-05-14 19:53:11
    Mkuu wa Mkoa wa Tanga, nchini Tanzania ,Martin Shigella amesema baada ya kufanya uchunguzi amebaini kuwa mpaka wa Lungalunga kwa upande wa Kenya haujafungwa ila wameongeza taratibu za kuvuka mpaka huo, hivyo amewataka maofisa wa Kituo cha Horohoro na kwa upande wa Lungalunga kutoa ushirikiano ili kulimaliza tatizo vizuri la kukwama kwa muda mrefu kwa magari ya mizigo yanayokwenda Mombasa, Kenya kutokea nchini humo .

    Uchunguzi alioufanya Shigella umetokana na zaidi ya magari 10 ya abiria na magari 40 ya mizigo yaliyokuwa yakisafiri kwenda Mombasa nchini Kenya, kuzuiwa katika mpaka wa Lungalunga upande wa Kenya hadi abiria na madereva wapimwe virusi vya corona na kusubiri majibu kwa muda wa siku tatu.

    Uamuzi huo umetokea usiku wa Jumatatu hadi Jumanne ambako hatua imesababisha baadhi ya Watanzania hao kugomea vipimo vya corona vya Kenya hadi kuwepo madaktari Watanzania.

    Kutokana na hali hiyo, baadhi ya abiria waliokuwa wakienda Mombasa waligoma kupima na kuamua kurudi Tanga.

    Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Shigella alifanya ziara mpakani hapo kujionea hali halisi.

    Aliwasisitiza maofisa wa Horohoro kutoa ushirikiano na wenzao wa Kenya bila kuathiri taratibu za mipaka za Tanzania na Kenya ili kuondoa changamoto hiyo pamoja na kuweka tahadhari za kujikinga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako