• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SHAMBULIZI: Kiungo wa Tottenham, Dele Alli avamiwa na wezi nyumbani kwake

  (GMT+08:00) 2020-05-15 08:20:28

  Kiungo wa Tottenham, Dele Alli amevamiwa na wezi Jumatano asubuhi waliokuwa na visu mikononi wakati akiwa nyumbani kwake Kaskazini mwa London. Ilielezwa kuwa katika jumba hilo, kulikuwa na watu watano, akiwemo kiungo huyo wa Kimataifa wa Uingereza, kaka wa Alli, marafiki zao wa kike na rafiki mwingine pia alikuwepo. Polisi walithibitisha kwamba walioshambulia nyumba hiyo ni wanaume wawili na ripoti zilidai Alli alikuwa mmoja wa wale walioshambuliwa. Polisi walisema kwamba hakuna mtu aliyekamatwa kwa sasa, lakini uchunguzi unaendelea juu ya tukio hilo. Polisi wanasema watu wawili wanaume katika nyumba hiyo walipata majeraha madogo usoni baada ya kushambuliwa. Pia wamesema wezi wawili waliingia katika nyumba huyo na kuiba vito vya thamani kabla ya kukimbia. Klabu ya Tottenham kupitia msemaji wao, walisema, wanamhimiza mtu yeyote mwenye taarifa yoyote awasiliane na polisi ili kusaidia uchunguzi wa tukio hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako