• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afrika CDC: Wataalamu wa matibabu wa China waisaidia Afrika kupambana na COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-05-15 09:22:33

  Kituo cha CDC cha Afrika kimesema wataalamu wa matibabu wa China wanazisaidia nchi za Afrika kupambana na COVID-19.

  Mkurugenzi wa kituo hicho Bw. John Nkengasong amesema wataalamu wa matibabu kutoka nchi 32 za Afrika hivi karibuni walifanya kongamano kwa njia ya mtandao wa Internet na wenzao wa China kuhusu namna ya kupambana na virusi vya Corona barani humo, na kujadili matibabu ya wagonjwa wa COVID-19 mjini Wuhan na dawa za jadi za China zikiwa tiba mbadala.

  Pia amesema katika wiki iliyopita, kituo cha CDC cha Afrika kiliendesha semina ya tisa ya kila wiki kuhusu mpango wa kimatibabu inayohudhuriwa na watu 312 kujadili njia zilizopo za kutibu COVID-19.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako